Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Sudan lagoma kuachia madaraka licha ya kusaini makubaliano

Sudan Pic Jeshi la Mapinduzi Sudan lagoma kuachia madaraka

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya mgawanyo wa madaraka uliofikiwa zaidi ya miaka miwili nchini Sudan, inaelezwa kuwa Jeshi la nchini humo bado linatawala kwa asilimia kubwa kuliko utawala wa kiraia.

Jeshi hilo lilifanya mapinduzi mwaka 2019 na kumtoa rais Omar-al- Bashir kufuatia maandamano ya raia yaliyofanyika kwa zaidi ya mwezi mmoja kuupinga utawala wa Rais huyo.

Viongozi wa jeshi la mapinduzi walisaini mkataba wa makubaliano wa miezi minne kuruhusu serikali ya mpito ya kiraia katika kipindi hicho cha kubadili utawala wa Rais huyo.

Wachambuzi wa Siasa wa kimataifa na wale wa ndani, wamesema kuwa Jeshi hilo bado linatawala kwa sehemu kubwa huku serikali hiyo ya mpito ikiwa haina nguvu ya kufanya maamuzi yahusuyo taifa kwa ujumla.

Hata hivyo hali ya uchumi nchini humo inatajwa kuzorota, huku famili nyingi zilizopata atahari katika mapinduzi hayo ya mwaka 2019 zikiwa zimeachwa bila malipo ya fidia, halii inatajwa kusababishwa na Serikali kukosa nguvu yake ya utawala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live