Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Sudan Kusini lanza kuondoka mashariki mwa DRC

Jeshi La Sudan Kusini Lanza Kuondoka Mashariki Mwa DRC Jeshi la Sudan Kusini lanza kuondoka mashariki mwa DRC

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Majeshi ya Sudan Kusini yaliyokuwa yakihudumu mashariki mwa DRC katika kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki EACRF, yameanza kuondoka mashariki mwa DRC Ijumaa hii.

Mapema Leo, kikosi cha kwanza cha Sudan kusini kimeoondoka Goma huku kingine kikitarajiwa kuondoka baadae Leo.

Leo tarehe nane Desemba ni siku ambayo amri ya kuhudumu ya kikosi cha jumuiya ya Afrika mashariki kuhudumu mashariki mwa DRC ilitolewa.

Amri hii iliongezwa kwa miezi mitatu mwezi septemba na kikao cha Marais wa EAC. Iliwahi tena kuongezwa mara mbili awali baada ya amri hiyo iliyotazamiwa kuwa kwa miezi sita kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.

Mapema wiki hii majeshi ya Kenya yalianza kuondoka DRC kupitia uwanja wa ndege wa Goma.

Jumatano wiki hii wakuu wa majeshi ya EAC walikutana Arusha Tanzania na kuafikiana kwamba shughulinzima ya kuondoka itakamilika mwezi Januari mwaka wa 2024 huku taarifa kamili kuhusu kitakachofanyika katika muda huo ikitarajiwa kutangazwa na wakuu hao.

DRC ilijiunga na EAC mwaka wa 2022 na mwishoni mwa mwaka huo kikosi cha kijeshi cha jumuiya hiyo kikaingia Mashariki mwa taifa hilo kudumisha amani.

Hatahivyo serikali ya Kinshasa ilitangazwa kutoridhishwa kwake na aliyekuwa mkuu wa kikosi hicho Meja Jenerali Jeff Nyaga na kudai kwamba alikuwa anaegemea upande wa M23 , hali ambayo ilichangia kuondoka kwake na kuletwa kwa Meja Jenerali Alfxard Kiugujambo ambalo pia halikukubaliwa mara moja na Kinshasa.

Kikosi hicho kimekabiliwa na hali ngumu ya maandamano dhidi yake huku raia mjini Goma wakikitaka kuondoka kwa kusema kimeshindwa kutekeleza majukumu ya kukabiliana na M23.

Baada ya mwaka mmojakikosi hicho kinaondoka ila kinajivunia kuhakikisha kwamba hali ya amani ilidumishwa kwa miezi saba huku M23 ikiondoka maeneo ya raia na kuingia maeneo waliyokubaliana kukaa katika mkataba wa Luanda wa 2022.

Ila katika miezi mitatu iliyopita hali ya usalama imekuwa mbaya wakati ambapo mapigano yamezuka kati ya M23 na kundi la wazalendo ambalo linaunga mkono serikali.

Katika wiki hii jeshi la FARDC la DRC limekabiliana na M23 mjini Masisi huku taarifa za hivi karibuni zikisema kwamba huenda mji wa Mushaki unakabiliwa na mapigano makalina inaripotiwa M23 imeingia katika mji huo.

Chanzo: Bbc