Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Somalia laua makumi ya al-shaabab

Somalia AU AU Jeshi la Somalia laua makumi ya al-shaabab

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabaab wameuawa katika operesheni za jeshi la Somalia.

Kundi hilo ambalo lina mielekeo na mafungamano ya itikadi kali na al-Qaeda, limekuwa likijaribu kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2007 na limefanya operesheni nyingi za kigaidi na kuua idadi kubwa ya wanajeshi na raia nchini humo na katika nchi jirani.

Ijumaa usiku, wanachama 120 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab waliuawa wakati wa operesheni za kijeshi katika eneo la Madag, katikati na Shabelle ya Kati iliyoko kusini mashariki mwa Somalia.

Dawood Uwais Jame, Waziri wa Habari wa Somalia, amethibitisha kwamba wapiganaji 100 wa al-Shabaab, ikiwa ni pamoja na viongozi kadhaa wa kundi hilo, wameuawa katika operesheni ya jeshi la Somalia katika eneo la Madag.

Akizungumzia kunaswa silaha na risasi za al-Shabaab katika operesheni hiyo, amesema, baada ya shambulio la vikosi vya jeshi, wanachama kadhaa wa kundi hilio la kigaidi walifanikiwa kukimbia.

Jeshi la Somalia

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanachama 20 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab wameuawa katika operesheni nyingine katika eneo la Shabul ya Kati.

Al-Shabaab ni kundi lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaeda na limefanya operesheni nyingi za kigaidi ambazo zimeua mamia ya watu barani Afrika.

Magaidi wa al-Shabaab wameshambulia mara kwa mara wanajeshi wa serikali na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika, pamoja na watu wa kawaida huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na kufanya operesheni kadhaa za umwagaji damu katika maeneo mengine barani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live