Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Rwanda 'limehuzunishwa' kufuatia kifo cha mwanajeshi wake

Jeshi La Rwanda Jeshi la Rwanda 'limehuzunishwa' kufuatia kifo cha mwanajeshi wake

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi la Rwanda linasema "limehuzunishwa sana" na kifo cha mmoja wa wanajeshi wake waliouawa na "watu wenye silaha" wakati wakishika doria na vikosi vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Shambulio dhidi ya vikosi hivyo lilitokea Jumatatu katika mkoa wa Haute-Kotto kaskazini-mashariki mwa CAR, Umoja wa Mataifa unasema katika taarifa.

"Watu watatu wenye silaha waliuawa na mmoja alitekwa," inaendelea kusema taarifa hiyo.

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, Valentine Rugwabiza, amelaani shambulio hilo dhidi ya walinda amani hao, na kulitaja kuwa la "kuudhi".

Wapiganaji wa Rwanda ni takriban wanajeshi 2,000 kati ya wanajeshi 17,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini CAR.

Rwanda pia ina takriban wanajeshi 2,000 nchini CAR waliotumwa kwenye makubaliano yanchi hizo mbili.

Wanajeshi hawa, pamoja na mamluki wa Urusi Wagner, walichukua jukumu muhimu katika kuwafukuza waasi waliotishia kuuteka mji mkuu, Bangui, mnamo 2021.

Chanzo: Bbc