Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Rwanda lamuua mwanajesho wa Congo

Mauaji Jeshi.jpeg Jeshi la Rwanda lamuua mwanajesho wa Congo

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wa Rwanda wamemuua kwa kumpiga risasi Mwanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alivuka mpaka kati ya nchi hizo mbili hapo jan, taarifa hii imethibitishwa na Wizara ya Ulinzi ya Rwanda na Jeshi la Congo.

Taarifa iliyochapishwa na DW Kiswahili imesema Mamlaka za Rwanda zimesema Mwanajeshi huyo aliwasili katika eneo la Rubavu na kuanza kuwafyatulia risasi Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi.

Msemaji wa Jeshi la Congo, Kanali Guillaume Ndjike amesema Askari huyo alijiunga na Jeshi hivi karibuni na huenda alipotea katika eneo hilo la mpakani wakati wa doria ya usiku huku akisema kuwa uchunguzi unaendelea.

Mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya Kongo na Rwanda. Siku ya Ijumaa rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana juu ya umuhimu wa waasi wa M23 kusitisha mapigano na kujiondoa katika maeneo wanayoyadhibiti mashariki mwa Kongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live