Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Nigeria lakanusha ripoti ya njama ya mapinduzi

Jeshi La Nigeria Jeshi la Nigeria lakanusha ripoti ya njama ya mapinduzi

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Nigeria limekanusha ripoti ya madai ya kuwepo njama ya mapinduzi ya kijeshi, likisema "madai hayo ni ya uongo kabisa" na kutangaza kuwa linachukua hatua kwa wale wanaohusika na uvumi huyo 'usio wa kizalendo."

Msemaji Jeshi Brigedia Jenerali Tukur Gusau katika taarifa yake aliashiria ripoti ya Jumapili ya chombo cha habari cha Sahara Reporters, ambacho kilidai kuwa kikosi maalumu cha Gadi ya Walinzi kimewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia mienendo isiyo ya kawaida jeshini, ripoti ambayo imesababisha tuhuma za njama ya mapinduzi ya kijeshi nchini Nigeria.

Jarida hilo la mtandaoni limeandika kuwa kuwepo tetesi za njama za mapinduzi ya kijeshi kulipelekea kufanyika mkutano wa dharura uliohusisha Rais Bola Tinubu, mkuu wa majeshi na kamanda wa Gadi ya Walinzi.

Gusau alisema katika taarifa yake kwamba: "Makao Makuu ya Ulinzi yanapenda kueleza wazi kwamba madai hayo ni ya uwongo kabisa. Ili kuepusha shaka, Gadi ya Walinzi kisheria huwa na jukumu la kulinda kiti cha madaraka (Urais) na mji mkuu pamoja na viunga vyake. Kwa hivyo, ikumbukwe kwamba Gadi ya Walinzi kila mara kimekuwa katika hali ya tahadhari ili kutekeleza vyema kazi walizopewa," Rais Bola Tinubu

Taarifa hiyo ilisema Mkuu wa Majeshi Jenerali Christopher Musa katika vikao mbalimbali "amesisitiza kujitolea Wanajeshi wa Nigeria katika kulinda na kudumisha demokrasia nchini Nigeria," na kwa hiyo, Makao Makuu ya Ulinzi "yanalaani vikali madai haya yasiyo na uthibitisho ambayo ni mawazo tu ya mchapishaji na hivyo wananchi wanapasywa kuyapuuza."

Aidha ametoa wito kwa vyombo husika vya usalama kuchukua hatua zinazofaa mara moja dhidi ya waandishi habari wa Sahara Reporters kwa "hatua hii isiyo ya kizalendo."

Taarifa hiyo imesema Jeshi la Nigeria litachukua kisheria kuhusu suala hilo ambalo lina nia mbaya ya kuleta mvutano usio wa lazima nchini."

Tangu Nigeria ipate uhuru mwaka wa 1960, kumekuwa na mapinduzi matano ya kijeshi katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika

Chanzo: www.tanzaniaweb.live