Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Nigeria laapa kulipiza kisasi baada ya wanajeshi kuuawa

Jeshi La Nigeria Laapa Kulipiza Kisasi Baada Ya Wanajeshi Kuuawa Jeshi la Nigeria laapa kulipiza kisasi baada ya wanajeshi kuuawa

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Jeshi la Nigeria limeapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanajeshi sita waliovamiwa wakiwa kwenye misheni ya amani katika jimbo la kati la Niger wiki iliyopita.

Wanajeshi hao walikuwa kwenye "doria" katika kijiji cha Karaga eneo la Shiroro Ijumaa iliyopita walipovamiwa na wale ambao jeshi liliwaita "magaidi".

Taarifa ya jeshi ilisema idadi ya washambuliaji wameuawa, na wengine bado wanafuatiliwa.

Iliapa kwamba "tukio hilo la kusikitisha litalipizwa kisasi na wanajeshi".

Wanajeshi waliouawa ni pamoja na maafisa wakuu wawili na wafanyikazi wengine wanne, kulingana na jeshi.

Maafisa wawili walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo.

Jeshi halijathibitisha taarifa za ndani kwamba afisa mmoja alitekwa nyara.

Haijabainika ni nani alitekeleza shambulio hilo lakini magenge yenye silaha, yanayojulikana na wenyeki kama majambazi, yamelaumiwa kwa kulenga vikosi vya usalama katika mashambulizi ya hivi majuzi.

Haya yanajiri wakati Nigeria ikiwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa siku mbili wa ngazi ya juu wa Afrika dhidi ya ugaidi katika mji mkuu wa Abuja.

Shambulizi hilo la kuvizia pia linafanyika wiki chache baada ya wanajeshi wengine 16 kuuawa walipokuwa wakijibu mapigano kati ya jamii zinazohasimiana katika jimbo lenye utajiri wa mafuta kusini mwa Delta.

Nigeria imekumbwa na wimbi la utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidia, pamoja na kupambana na makundi mbalimbali ya wanajihadi.

Chanzo: Bbc