Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Mapinduzi Guniea la waachia huru zaidi ya viongozi 70 wa Upinzani

Guniea 23 Jeshi la Mapinduzi Guinea la waachia huru viongozi zaidi ya 79 wa upinzani

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Mapinduzi nchini Guinea, limewaachia huru Wanasiasa wa upinzani zaidi ya 79 waliokuwa wakitumikia vifungo katika mji wa Conakry nchini humo.

Hatua hii inakuja wakati Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ikiwa katika mchakato wa kukutana kujadili mwenendo wa kidemokrasia na usalama nchini humo pamoja na kushinikiza kuachiwa kwa Rais Aplha Conde aliyetolewa madaraka na jeshi hilo Septemba 05, 2021.

Mwanasheria anaye shughulikia kesi za viongozi hao, amethibitisha taarifa hii kwa kusema kuwa tayari washitakiwa 79 wamesharuhusiwa kutoka mara baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa jeshi hilo.

Hata hivyo Jeshi hilo liliitaka Mahakama kuhakikisha inaharakisha upatikanaji wa haki ikiwa ni pamoja na kuwaachia huru wanasiasa hao ambao kwa mujibu wao ni wameshtakiwa kinyume cha sheria

Chanzo: www.tanzaniaweb.live