Nchini Mali, watu 25 waliuawa na jeshi la Mali na wasaidizi wake kutoka kundi la Wagner. Ilikuwa Januari 26, katika kijiji cha Welingara, ambacho pia huitwa Wuro Ferro katika lugha ya Kifulani.
Kijiji ambacho kinapatikana katika eneo la Nara, karibu na mpaka wa Mauritania, eneo ambalo jeshi la Mali limekumbwa na mashambulizi kadhaa ya wanajihadi katika wiki za hivi karibuni.
Wanajeshi wa Mali na washirika wao kutoka Urusi wa kundi la mamluki la Wagner walifika asubuhi na mapema, wakakamata wanaume 25 na wavulana wadogo, na kuwapeleka kilomita 2 kutoka kijiji hicho. Hapa ndipo, kwa mujibu wa vyanzo vingi vya ndani vilivyohojiwa na RFI, miili hiyo ilipatikana, ikiwa imerundikana juu ya kila mmoja, wengine wakiwa wamezibwa macho, wakiwa wamejawa na risasi au makoo yaliyopasuliwa, na wengi walichomwa.
Wahanga hao wakiwemo watoto wote ni kutoka jamlii ya Fulani. Vyanzo kadhaa vya kijamii vinaendelea kushutumu "kulegwa kwa watu kutoka kabilia moja".