Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Mali latangaza kumuua Afisa Mkuu wa Islamic State

Mali Armyy Jeshi la Mali latangaza kumuua Afisa Mkuu wa Islamic State

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi nchini Mali limetangaza katika Televisheni kumuua Afisa Mkuu wa kundi la Islamic State Abou Houzeifa, katika eneo la Ménaka Kaskazini Mashariki mwa Mali.

Jeshi la Mali linadai kuwa hayo ni mafanikio mapya katika vita dhidi ya jihadi katika kukomesha adui wa amani wa nchi ya Mali na meneo mengine jirani.

Taarifa kutoka kwa Jeshi la Mali zilithibitisha kwamba kitambulisho na ushahidi uliokusanywa zinathibitisha kifo cha Abou Houzeifa, Gaidi maarufu wa kigeni ambaye alifanya dhuluma kadhaa dhidi ya raia wasio na hatia na mashambulizi dhidi ya vikosi vya kijeshi vya Muungano wa Sahel na majeshi ya kigeni.

Mnamo Oktoba 4, 2017, Wanajeshi tisa kutoka Marekani na watano wa Niger waliuawa katika shambulio la kuvizia lililotekelezwa na wanajihadi karibu na Tongo, kilomita ishirini kutoka mpakani mwa Mali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live