Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la DR Congo lazima jaribio la mapinduzi

Tshisekedi Rais Felix Tshikedi

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuzuia jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Felix Tshikedi jijini Kinshansa.

Taarifa hiyo iliyochapishwa katika tovuti ya BBC leo Jumapili Mei 19, 2024 imesema; “Msemaji wa jeshi la DR Congo, Brigedia Jenerali Sylavin Ekenge amesema kwenye kituo cha runinga cha Taifa, RTNC TV kwamba washukiwa kadhaa wamekamatwa na hali sasa imedhibitiwa.

“Jaribio la mapinduzi limezimwa na vikosi vya ulinzi na usalama wa taifa. Jaribio hilo lilihusisha raia wa kigeni na baadhi yao walikuwa ni raia Wa Congo.”

Taarifa ya kuzimwa kwa jaribio hilo imetolewa saa chache baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba ya Vital Kamerhe ambaye ni mkuu wa zamani wa majeshi na mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi.

Rais Tshisekedi hajatoa tamko lolote kuhusu tukio hili hadi sasa.

Hayo yanajiri huku kukiwa na mzozo unaokikumba chama tawala cha Rais Felix Tshisekedi kuhusu uchaguzi wa uongozi wa Bunge ambao ulipaswa kufanyika Jumamosi lakini ukaahirishwa.

Balozi wa Japan katika mji mkuu wa Congo amewaonya Wajapani walioko DRC kutotoka nje.

Chanzo: Mwananchi