Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi Uganda lamkamata fundi wa Mabomu Al-Iraq

WhatsApp Image 2024 05 19 At 09.jpeg Jeshi Uganda lamkamata fundi wa Mabomu Al-Iraq

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Uganda limethibitisha kumkamata kamanda wa kundi la waasi la ADF linaloshirikiana na kundi linalojiita dola ya kiislamu, ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza mabomu yanayotumiwa na kundi hilo kufanya mauaji.

Kamanda huyo Anywari Al-Iraq ambaye ni raia wa Uganda, alikamatwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalipo maskani ya kundi la hilo.

Katika operesheni ya kumsaka watu tisa wakiwemo watoto waliokolewa kutoka katika eneo hilo lililopo mkoani Ituri Mashariki mwa DRC, huku bidhaa mbalimbali za kutengenezea mabomu zikikamatwa.

Kundi hilo la waasi wa ADF lilianza harakati zake nchini Uganda lakini limekuwa na ngome yake nchini Congo tangu miaka ya 90.

Lilitangaza kushirikiana na kundi linalojiita dola la kiislamu mwaka 2019 na linatuhumiwa kufanya mauaji ya mamia ya wanavijiji katika mashambulizi ya mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live