Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi Sudan lawataka RSF kuondoka maeneo ya raia

Sudan Yataka Kurejeshewa Uanachama Kabla Ya Kukubali Upatanishi Wa AU Jeshi Sudan lawataka RSF kuondoka maeneo ya raia

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jenerali mwandamizi wa Jeshi la Sudan, Yasser al-Atta, amesema hakutakuwa na usitishaji vita nchini Sudan katika mwezi mtukufu wa Ramadhani isipokuwa kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) litaondoka kwenye makazi na maeneo ya raia.

Kauli hiyo inafuatia ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kusitisha mapigano nchini Sudan katika mwezi wa Ramadhani ambalo limekaribishwa na RSF.

Taarifa iliyotolewa na Jenerali Al-Atta, kwenye jukwaa la kijamii la Telegram pia imeashiria maendeleo ya hivi karibuni ya jeshi la Sudan huko Omdurman.

Taarifa hiyo imesema: Hakuwezi kuwa na usitishaji wa vita mwezi Ramadhani isipokuwa pale RSF itakapotekeleza ahadi iliyotolewa Mei mwaka jana katika mazungumzo ya Jeddah huko Saudi Arabia ya kuondoka kundi hilo katika makazi ya raia na vituo vya umma.

Vilevile imesema kuwa, kiongozi wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo, hapaswi kuwa na nafasi yoyote katika siasa za baadaye za Sudan au katika jeshi la nchi hiyo.

Kauli hiyo inafuatia ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) la kuasitishwa mapigano nchini Sudan wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ulioanza leo katika baadhi ya nchi za Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres aliwataka majenerali wa kijeshi nchini Sudan waheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusitisha vita haraka ndani ya mwezi huo mtukufu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live