Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo laporomoka baada ya wapangaji kuhama Kenya

FiEBNzrXoAA  OP Jengo laporomoka baada ya wapangaji kuhama Kenya

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Jengo la makazi la gorofa tano liliporomoka Jumatatu huko Ruiru viungani mwa mji mkuu, Nairobi, siku moja tu baada ya wapangaji wake kuhamishwa.

Uhamisho huo ulishuhudiwa na gavana wa eneo hilo, Kimani Wamatangi, Jumapili baada ya jengo hilo kupata nyufa.

Ilikuwa na wapangaji zaidi ya 100, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Hapo awali Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi (NCA) iliripotiwa kulipata jengo hilo na kasoro za kimuundo.

Kituo cha runinga cha Citizen TV kimetuma picha ya jengo hilo kwenye Twitter:

Chanzo: Bbc