Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali wa zamani wa Congo Norbert Dabira aachiliwa huru

Jenerali Wa Zamani Wa Congo Norbert Dabira Aachiliwa Huru Jenerali wa zamani wa Congo Norbert Dabira aachiliwa huru

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: Voa

Jenerali Norbert Dabira, aliyewahi kuwa karibu na rais mkongwe wa Kongo Denis Sassou Nguesso ametolewa jela baada ya kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa madai ya kupanga njama za mauaji, familia yake ilisema.

Jenerali Dabira, mwenye umri wa 73, alikuwa mmoja wa viongozi watatu wa ngazi za juu waliofungwa gerezani mwaka 2018, wengine ni waliokuwa wagombea urais Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko na waziri wa zamani Andre Okombi Salissa.

Dabira aliachiliwa siku ya Jumatatu, mmoja wa ndugu zake alisema.

“ Polisi walikuja na kumshusha nyumbani. Tulikuwepo wengi wakati alipowasili, alivaa suti na tai” chanzo cha habari hii kilisema Jumatatu jioni, akiomba jina lake lisitajwe.

Dabira aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 80, ambaye amekuwa katika madaraka huko Jamhuri ya Kongo, ambayo pia ikijulikana kwa jina la Congo-Brazzaville, kwa kipindi cha miaka 39.

Jenerali Dabira alihukumiwa kifungo kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa ndani wa taifa, akishutumiwa kukodisha "wanajeshi maalum wenye shabaha ya hali ya juu" ili kuiangusha ndege ya Sassou Nguesso.

Kabla ya kutofautiana na Sassou Nguesso, Dabira aliwahi kuchunguzwa nchini Ufaransa kwa kuhusika na kutoweka kwa watu 350 waliokuwa wamerejea Congo-Brazzaville mwaka 1999 kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako walikuwa wamepewa hifadhi kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu.

Chanzo: Voa