Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali wa Sudan akataa pendekezo lililoongozwa na Kenya

Jenerali Wa Sudan Akataa Pendekezo Lililoongozwa Na Kenya Jenerali wa Sudan akataa pendekezo lililoongozwa na Kenya

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: Voa

Jenerali mmoja wa Sudan akataa pendekezo lililoongozwa na Kenya kwamba walinda amani wa Afrika Mashariki wasaidie kumaliza vita vya zaidi ya siku 100 nchini Sudan

Jenerali mmoja wa Sudan alikataa akitoa lugha ya vitisho pendekezo lililoongozwa na Kenya kwamba walinda amani wa Afrika Mashariki wasaidie kumaliza vita vya zaidi ya siku 100 nchini Sudan katika video iliyotolewa Jumatatu na kukosolewa vikali na mamlaka ya Kenya.

Mapigano hayo ya Jeshi la Sudan na vikosi vya RSF yamepokea maombi mengi ya upatanishi wa kimataifa lakini hakuna waliofaulu kukomesha au hata kusitisha kwa kiasi kikubwa mapigano hayo yaliyozuka tangu Aprili 15

Mapema mwezi huu IGAD jumuiya ya kanda ya Afrika Mashariki ambayo Kenya ni mwanachama ilipendekeza mpango ambao utajumuisha kupelekwa kwa walinda amani katika mji mkuu Khartoum.

Jeshi la Sudan limekataa mara kwa mara mpango huo unaoongozwa na Kenya likishutumu mamlaka hiyo ya kikanda kuunga mkono vikosi vya RSF.

Chanzo: Voa