Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali wa Sudan aichimba mkwara Kenya

Yassir AlAtta Jenerali wa Sudan, Yassir al-Atta.

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jenerali wa Sudan, Yassir al-Atta, amekataa kwa lugha ya vitisho pendekezo linaloongozwa na #Kenya la kupeleka Wanajeshi wa kulinda amani wa Afrika Mashariki, kusaidia kumaliza vita kati ya Serikali na vikosi vya RSF ambavyo vimedumu kwa zaidi ya siku 100.

Katika video iliyoachiwa Julai 25, 2023, Jenerali huyo amenukuliwa akisema, "Waache vikosi vya Afrika Mashariki wabaki walipo. Leteni jeshi la Kenya... Nawaapia, hakuna hata mmoja wao atakayerejea akiwa hai."

Sudan imekuwa ikiishutumu Kenya kufadhili vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) ambavyo ni mahasimu wao, madai ambayo Kenya yameyakataa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live