Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali Nyamvumba ateuliwa kuwa balozi wa Rwanda nchini Tanzania

Jenerali Patrick Nyamvumbag Jenerali Patrick Nyamvumba.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Mawaziri nchini Rwanda limemuidhinisha Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa Balozi wa Rwanda nchini Tanzania.

Jenerali Nyamvumba amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Rwanda, Kamanda wa Kikosi cha Umoja baina ya AU na UN huko Darfur kwenye misheni ya ulinzi wa amani chini ya mwamvuli wa UNAMID.

Mhitimu huyo wa chuo cha Kijeshi cha Nigeria, ameshawahi pia kuwa Kamanda wa Vikosi vya Ardhini, Mkuu wa chuo cha Kijeshi na Rais wa Mahakama ya kijeshi nchini Rwanda.

Jenerali Patrick anachukuwa nafasi ya mwanamke Fatou Harerimana ambaye alikuwa amemaliza mwaka mmoja akiwa Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,kwasa akiwa ameteuliwa kuwa Balozi wa Rwanda nchini Pakistan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live