Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali Nguema akataa kulipwa mshahara wa Urais

Jen Nguema.png Jenerali Nguema akataa kulipwa mshahara wa Urais.

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi huyo wa Kijeshi ametangaza rasmi kuwa hatochukua Mshahara huo kwa muda wote atakaokuwa Madarakani isipokuwa ataendelea kupokea Mshahara wa Kamanda wa Jeshi, nafasi ambayo alikuwa akiitumikia kabla ya Mapinduzi yaliyomuondoa Ali Bongo.

Msemaji wa Serikali amesema Jenerali Nguema amechukua uamuzi huo kwa kuzingatia mahitaji ya dharura za Kijamii pamoja na matarajio mengi ya Watu kwa uongozi mpya wa Taifa hilo baada ya kuzorota kwa hali ya Uchumi.

Mbali na Mshahara wa Urais, Jenerali Nguema amepunguza matumizi ya Serikali ikiwemo kukata Posho za Wabunge na Posho za Vikao vya Wafanyakazi wa Serikali, hatua iliyotajwa kurejesha imani ya Wananchi kwa Uongozi mpya wa Gabon.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, utawala wa miaka 14 wa Rais Ali Bongo aliyeondolewa madarakani Agosti 2023, uligubikwa na Ufisadi, Rushwa, Ubovu wa Miundombinu ya Huduma Muhimu na Uminyaji wa Uhuru wa Kujieleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live