Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali Mabeyo atembelea Ubalozi wa Afrika Kusini

0b75f7e0c6f8db51208b30c7e1700a1e Jenerali Mabeyo atembelea Ubalozi wa Afrika Kusini

Sat, 29 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Jenerali Mabeyo yupo Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini, Jenerali SZ Shoki zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria.

Kuhudhuria sherehe hizi ni utaratibu uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha mashirikiano hususani katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo Ia nchi za SADC.

Jenerali Mabeyo alikaribishwa Ubalozini na Balozi Mej Jen. Gaudence Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi Balozi Milanzi alitoa taarifa fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho.

Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchiza eneo la uwakilishi ikiwa ni pamoja na SADC. Kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza kuendeleza Diplomasia ya kisiasa na kutekeleza Diplomasia ya uchumi.

Upande wake Jenerali Mabeyo alielezea ziara yake kwa ujumla nchini Afrika Kusini imekuwa ni ya mafanikio, na pia kuna mambo kama ambayo kama Mkuu wa Majeshi ameona yanafaa kuigwa ili kuboresha utendaji wa Jeshi la Tanzania.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amelenga kuendeleza maendeleo ndani na nje ya nchi mfano katika kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwelekeo unaelekeza kuimarisha Diplomasia kwa kujenga mahusiano na nchi duniani kwa kuimarisha Diplomasia ya siasa na Diplomasia ya uchumi.

Jenerali Mabeyo alimsihi Balozi na watumishi wa Ubalozi kuhakikisha kuwa wanaielewa na kuisimamia dira ya Diplomasia kama ilivyoainishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuweza kutelekeza majukumu yao kwa wepesi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz