Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali Katumba: Mshukiwa mkuu wa jaribio la mauaji auawa, wenzake 4 wakamatwa

282c0a92558fd767 Jenerali Katumba: Mshukiwa mkuu wa jaribio la mauaji auawa, wenzake 4 wakamatwa

Sat, 3 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Jenerali Katumba Wamala alipigwa risasi kwenye shambulio ambalo bintiye na dereva wake waliangamia Maafisa wa polisi nchini Uganda walifanikiwa kuwakamata washukiwa waliohusika na mauaji hayo Mshukiwa mkuu aliuawa baada ya kujaribu kukataa kukamatwa siku ya Alhamisi, Jula 1Uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa kufuatia shambulio hiloMaafisa wa polisi nchini Uganda wamefanikiwa kumuua mshukiwa mmoja na kuwakamata wengine wanne waliohusishwa na jaribio la mauaji kwa jenerali Katumba Wamala mnamo Juni, Mosi.

Katumba alipigwa risasi akiwa katika babarara ya Kisota wilayani Kisaasi, bintiye Nantogo Brenda na dereva wake Kayondo Haruna waliangamiaa kwenye shambulio hilo.

Kwenye taarifa ya polisi, mshukiwa Muhammad Kagugude almaarufu Bafumoya alikiri kuhusika kwenye mauaji hayo.

" Alifanya uchunguzi wa kina kuhusu alipokuwa na kila hatua aliyoichukua Jenerali Katumba, aliwafahamisha washukiwa wenzake na kwa haraka walimshambulia," Ilisoma taarifa ya polisi.

Baada ya kumuhoji Bafumoya kwa muda, maafisa wa polisi waliweza kuwakamata Walusimbi Kamada maarufu Mudinka ambaye anasemekana kuwa dereva aliyewabeba washambuliaji.

Bafumoya alipeana taarifa zaidi kuhusu yaliotendeka siku hiyo, aliwaonyesha maafisa wa polisi mahali kisa hicho kilitendeka na jinsi kilivyotekelezwa.

Polisi walifululiza hadi kijiji cha Kawanda ambapo walimkamata Kisambira Siriman maarufu Mkwasi ambaye aliripotiwa kupokea silaha kutoka kwa Lutwama Hussein almaarufu Master.

Wengine waliokamatwa ni Mustafa Kawawa Ramadan maarufu Amin au Musa akiwanyumbani kwake eneo la Maganjo wilayani Nabweru.

JeneraliWamala anaaminiwa kuwa kiongozi mwaminifu sana kwa Rais Yoweri Museveni kutokana na nyadhifa mbalimbali ambazo ametumikia nchi hiyo.

Museveni alilaani shambulio hilo na kuwaagiza maafisa wa polisi kufanya uchunguzi na kukabiliana vilivyo na waliohusika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke