Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jenerali Burhan: Vikosi vya RSF havitaki amani

Jenerali Burhan Jenerali Burhan: Vikosi vya RSF havitaki amani

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Baraza la Uongozi na Kamanda wa Jeshi la Sudan amesema kuwa hakutakuwa na chaguo jinjgine ghairi ya ufumbuzi wa kijeshi iwapo vikosi vya nchi hiyo vya msaada wa haraka (RSF) vitapinga taarifa ya Jeddah.

Jenerali Abdel Fattah al Burhan mkuu wa baraza la uongozi la Sudan na kamanda wa jeshi la nchi hiyo ambaye kwa wiki kadhaa sasa ameondoka Khartoum na kuelekea huko Port Sudan katika pwani ya Bahari Nyekundu juzi Jumanne aliwasili ghafla katika kambi ya kijeshi huko Omdurman (mashariki mwa Mto Nile) na akasema mbele ya hadhara ya vikosi vya ulinzi vya Sudan kwamba: Mazungumzo yanayohusiana na kusitisha mapigano yalianza tena tangu wiki jana kati ya jeshi na vikosi vya msaada wa haraka (RSF) huko katika mji wa Jeddah Saudi Arabia. Vikosi vya RSF vya Sudan

Al Burhan amebainisha kuwa: Kwa mujibu wa taarifa ya Jeddah ambapo iliafikiwa kuwa, vikosi vya RSF viondoke katika maeneo na majengo ya serikali yenye kuhudumia raia, wawakilishi wa jeshi la Sudan walielekea Jeddah mahali panapofanyika mazungumzo ya amani kwa upatanishi wa Marekani na Saudi Arabia na kwamba ameshiriki katika mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la Sudan Tribune, Jenerali Burhan amesisitiza kwamba jeshi halitalegeza kamba kwa vikosi vya RSF katika mazungumzo ya Jeddah, akisema: Hakuna mtu atakayetoa ridhaa kwa majambazi, wauaji na watu wanaovamia nyumba za watu. Ameongeza kuwa: Jeshi la Sudan linataka amani na kustafidi na njia za amani ili kuhitimisha mapigano na vikosi vya msaada wa haraka. Jenerali Abdel Fattah al Burhan mkuu wa baraza la uongozi la Sudan amebainisha kuwa: Ikiwa upande wa pili haukubali mchakato huu, basi jeshi pia halina chaguo jingine ila kutumia suluhisho la kijeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live