Vyanzo mbalimbali vya habari vinathibitisha kuwa wazirimkuu wa zamani wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni Jumatatu amefikishwa katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri mjini Bujumbura.
Miongoni mwa waliothibitisha ni chombo cha kitaifa kinachohusika na haki za binadamu nchini Burundi, CNIDH.
Haijulikani ni lini aliletwa baada ya zaidi ya wiki mbili kuwa mikononi mwa taasisi ya uchunguzi.
Kupelekwa kwa Jenerali Bunyoni katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambayo kwa kawaida huwa karibu na ofisi ya Seneti, kulifanyika katika mazingira yenye ulinzi mkali .
Walioweza kupata mwanga wa tukio hilo wanasema waliona gari za pick-up zikimleta mtu ambaye alipelekwa ofisini muda mfupi baadaye na kurudishwa.
Haijulikani ni lini Jenerali Bunyoni alichukuliwa baada ya kuripotiwa kutoroka.
Hadi sasa, ofisi ya Mwanasheria mkuu imekuwa ikisema kuwa yuko mikononi mwa wachunguzi, lakini eneo aliko halijabainika. Jenerali Bunyoni alikamatwa tarehe 17 mwezi Aprili.
Katika taarifa yake, mwendesha mashitaka alisema alikamatwa akiwa mafichoni katika jimbo la Bujumbura baada ya vyombo vya usalama kumsaka na kumpoteza nyumbani kwake, ambapo walimtafuta kwa siku nne kabla.
Baada ya kukamatwa, Msemaji wa Mahakama, Agnes Bangiricenga, alitangaza kuwa Jenerali Bunyonizi anashitakiwa kwa makosa matatu, mkiwemo ukiukaji wa usalama na uharibifu wa mali ya taifa.