Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 52 kwa kumuua mtoto miaka 5 kwa tambiko

Jela Miaka 52 Kwa Kumuua Mtoto Miaka 5 Kwa Tambiko Jela miaka 52 kwa kumuua mtoto miaka 5 kwa tambiko

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama ya juu katika wilaya ya Iganga mashariki mwa Uganda imemhukumu mwanaume mmoja kwa kifungo cha miaka 52 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka 5 kwa tambiko za kishirikina.

Jaji David Batema, alitoa hukumu ya kufungwa kwa Hassana Kafudde pamoja na Issa Muyita ambaye alihukumiwa miaka 25 gerezani.

Issa ni baba wa marehemu Juma Muyita na anashutumiwa kwa kushirikiana na Kafudde kumua mtoto wake ambaye wakati alipoliuliwa alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Mirembe Junior katika eneo la Kawempe mnamo mwaka 2017.

Katika uamuzi wake, jaji Batema alibaini kuwa hukumu hiyo nzito ililenga kuzuia vitendo kama hivyo.

Watetezi wa haki za watoto nchini Uganda wameipongoza mahakama hiyo kwa uamuzi huo.

Chanzo: Bbc