Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela maisha kwa kujihusisha na mauaji kwa niaba ya Yahya Jameh

Jela Maisha Kwa Kujihusisha Na Mauaji Kwa Niaba Ya Yahya Jameh Jela maisha kwa kujihusisha na mauaji kwa niaba ya Yahya Jameh

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mwanaume mmoja raia wa Gambia nchini Ujerumani amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika kikosi cha mauaji kilichofanya kazi kwa niaba ya Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Bai L, alifanya kazi kama dereva wa kikosi hicho kinachojulikana kwa jina la "Junglers".

Alipatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji na jaribio la kuua.

Mnamo mwaka wa 2019, wakati wa kusikilizwa kwa Tume ya Ukweli, Maridhiano na Fidia ya Gambia (TRRC), wafuasi wengine watatu wa "Junglers" walimshtaki Bw Jammeh kwa kuamuru mauaji mengi, ikiwa ni pamoja na mauaji ya 2013 ya wafanyabiashara wawili wa Marekani, Gambia na mwanahabari mkongwe Deyda Hydara.

Miongoni mwa uhalifu ambao Bai L alishutumiwa nao ni kusaidia kusimamisha gari la Hydara kabla ya kuuawa na kumuendesha mmoja wa wauaji, shirika la habari la AFP linaripoti.

Baada ya miaka 22 kama rais, Bw Jammeh awali alikataa kuachia madaraka baada ya kushindwa katika uchaguzi mwaka wa 2016.

Hatimaye alikwenda uhamishoni baada ya nchi wanachama wa jumuiya ya kikanda kutuma wanajeshi kumshinikiza aondoke madarakani.

TRRC, ambayo ilianzishwa baada ya kuondoka, iliwasikiliza mamia ya mashahidi kuhusu vikosi vya unyongaji na madai mengine ya ukiukaji wa haki uliofanywa chini ya utawala wake.

Chanzo: Bbc