Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je kupeleka jeshi la Ecowas kutakomesha mapinduzi ya Niger?

Je Kupeleka Jeshi La Ecowas Kutakomesha Mapinduzi Ya Niger Je kupeleka jeshi la Ecowas kutakomesha mapinduzi ya Niger?

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Rais Mahamat Idris Deby wa Chad alifanya mazungumzo ya kina na kiongozi wa jeshi lililofanya mapinduzi wiki iliyopita nchini Niger.

Alikwenda nchini humo akiwa balozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kuwashawishi viongozi wa mapinduzi ya Niger kuondoka mamlakani na kumrejesha Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum kwenye kiti.

Hili ni moja ya maombi ambayo kundi la ECOWAS liliwasilisha kwa Niger.

Deby katika taarifa yake, pia alisema kwamba alizungumza na rais aliyeondolewa madarakani wa Niger ambaye bado anazuiliwa huko Niamey.

Chad ni jirani wa Niger upande wa mashariki, na ni rafiki yake mkubwa. Wote ni wanachama wa mashirika ya kijeshi na ya kiraia, ikiwa ni pamoja na Shirika la Maendeleo ya Ziwa Chad na Timu ya Kukabiliana na Mafuriko ya Jangwa la CILSS na Kikosi Kazi cha Pamoja dhidi ya Boko Haram MNJTF.

Kama jeshi lenye nguvu zaidi katika Sahel, Chad imeunga mkono Niger wakati wa mashambulizi ya jihadi katika miaka ya hivi karibuni.

Mahamat Deby anaweza kuwa mtu ambaye viongozi wa mapinduzi ya Niger watamuona bora zaidi. Yeye si rais aliyechaguliwa, ni kiongozi wa kijeshi ambaye alichukua madaraka baada ya kifo cha baba yake.

Na kwa kuwa si mwakilishi wa ECOWAS, jeshi la Niger linaweza kuiamini Chad kuwa ndiyo inayoweza kufuata haki ikiwa itaingilia kati mgogoro huu.

Hakuna taarifa za wazi juu ya athari za juhudi za Mahamat Deby, lakini inaonekana kwamba makataa ya siku saba na tishio la hatua za kijeshi vimewakatisha tamaa watawala wapya wa Niger.

Mtaalamu wa masuala ya usalama nchini Nigeria, Dk Kabir Adamu alisema uamuzi wa ECOWAS uliwashangaza kwa sababu shirika hilo halikuchukua uamuazi kama huo wakati wanajeshi waliponyakua mamlaka katika nchi za Mali, Burkina Faso na Guinea.

Hali imezidi kuwa ngumu kwa kundi hilo baada ya mataifa matano kati ya 15 wanachama kuasi jeshi katika miaka ya hivi karibuni.

Iwapo safari ya Deby itafanikiwa, wanajeshi wa Niger watakubali kurejea katika kambi hiyo, eneo la Afrika Magharibi ambalo limekuwa likikumbwa na mzozo wa wanamgambo wa jihadi kwa miaka mingi, na wataepuka kushiriki tena katika ghasia nyingine.

Mvutano uliongezeka siku ya Jumatatu mjini Niamey, baada ya jeshi tawala kumshutumu mshirika wake wa zamani Ufaransa kwa kujaribu "kuanzisha mashambulizi ya kurejesha Bazoum madarakani," kulingana na Reuters.

Chanzo: Bbc