Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaribio la kuchelewesha uchaguzi DR Congo lawakasirisha wapinzani

Jaribio La Kuchelewesha Uchaguzi DR Congo Lawakasirisha Wapinzani Jaribio la kuchelewesha uchaguzi DR Congo lawakasirisha wapinzani

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeelezea kughadhabishwa na "jaribio" la Rais Felix Tshisekedi kuahirisha uchaguzi mkuu wa Disemba 20 kutokana na kuendelea kukosekana kwa usalama mashariki mwa nchi.

"Hali ya mashariki mwa nchi haipaswi kuwa kisingizio cha rais kuahirisha uchaguzi," Cherubin Okende, msemaji wa mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi alinukuliwa na shirika la utangazaji la Ufaransa RFI akisema.

Bw Okende alimkumbusha Bw Tshisekedi kuhusu ahadi aliyoitoa siku za mwanzoni mwa urais wake ya kuanzisha makao makuu ya jeshi mashariki mwa nchi katika juhudi za kukabiliana na makundi yenye silaha.

"Miaka minne baadaye, serikali bado hajaweza kurejesha amani katika eneo hili la nchi," alisema.

Kiongozi wa upinzani Martin Fayulu, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 70 cha katiba, rais anachaguliwa kwa muhula wa miaka mitano.

"Ikifika tarehe 23 Januari 2024, Tshisekedi lazima aondoke katika wadhifa wake," alisema.

Wanasiasa hao wawili wa upinzani walikuwa wakijibu maelezo ya Bw Tshisekedi kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuwa mzozo wa mashariki unaweza kuchelewesha uchaguzi.

Hata hivyo wakosoaji wanaamini kuwa changamoto mbalimbali zinaweza kutumika kama kisingizio cha muungano unaotawala kuhalalisha kuhairishwa kwa uchaguzi.

Chanzo: Bbc