Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Janeth Museveni agoma kufungua shule za kimataifa Uganda

Janet Musevenwwww Janeth Museveni, Waziri wa Elimu na Michezo Uganda

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Elimu na Michezo wa Uganda, Janet Museveni, ambaye pia ni Mke wa Rais wa nchi hiyo, amekataa ombi la balozi wa Ubelgiji la kufungua shule za kimataifa kabla ya mwisho wa mwaka.

Balozi Rudi Veestraeten alitoa ombi hilo kwa Serikali kufuatia kalenda ya masomo inayotumiwa na wanafunzi wa shule hizo na kusema kuwa mwaka wa masomo unapaswa kuanza mwezi Septemba tofauti na masomo ya Uganda yanayoanza mwezi Januari.

Ameongeza kusema kuwa, kama shule hizo zitalazimika kufunguliwa mwezi Januari sambamba na shule za Serikali basi wanafunzi wa shule hizo watapoteza masomo yao kwa nusu mwaka.

Hata hivyo Waziri huyo amekataa ombi hilo kwa kigezo cha kuwa wanafunzi wa shule za kimataifa wengi wanasoma masomo ya kutwa hivyo ni rahisi kusambaza virusi vya Corona.

"Nimepokea barua kutoka kwa balozi mwingie nae anaomba tufungue shule hizi za kimataifa, shida ni moja, wanafunzi hawa watasambaza virusi vya Corona kutoka mashuleni hadi majumbani, tutaiambia nini jamii ?"amesema Waziri huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live