Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Janeth Magufuli aonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu mumewe alipozikwa

3f83de9129021085 Janeth Magufuli aonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu mumewe alipozikwa

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mama Janeth Magufuli alikuwa akihudhuria misa takatifu iliyokuwa ikifanyika katika Kanisa Katoliki la St Peters jijini Dar es Salaam

- Misa hiyo iliandaliwa kuadhimisha siku ya 40 tangu kifo cha Magufuli kilichotokea Machi 17

- Janeth aliandamana na Mary Majaliwa, mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

Mama Janeth Magufuli amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu mumewe mumewe, John Pombe Magufuli kuzikwa.

Haya yanajiri wiki moja baada ya habari kuibuka kuwa Mama Janeth alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kupatwa na mshtuko uliotokana na kumpoteza mumewe.

Janeth aliungana na waumini wa Kanisa Katoliki la St Peters Oysterbay jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku 40 tangu Magufuli alipofariki dunia.

Mama Janeth alikuwa ameandamana na makasisi katika kanisa hilo, na Mama Mary Majaliwa, mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, miongoni mwa wengine.

Jumapili, Aprili 18, kifungua mimba wa Janeth, Joseph Magufuli alithibitisha kuwa mamake alikuwa mgonjwa baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo kufuatia kifo cha mumewe, ambaye pia alikuwa rais wa tano wa Tanzania.

Joseph alikuwa amewakilisha mamake wakati wa hafla ya kutoa shukrani kwa utawala wa Rais Samia Suluhu, makasisi, kikosi cha usalama kwa msaada wao katika kipindi kigumu walipofiwa na baba yao.

Alisema mama yake (Mama Janeth) alikumbana na shida za kiafya baada ya kupata mshtuko kidogo kufuatia kifo cha Magufuli.

"Yeye ni mgonjwa lakini anapokea matibabu. Ameniuliza nitoe shukrani zake kwa Watanzania kwa pole na ushirikiano wao mara tu baada ya kutangazwa kwa kifo cha baba yetu hadi kuzikwa kwake mwishoni mwa mwezi uliopita," Joseph alisema.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke