Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamhuri ya Afrika ya Kati yatafuta mamluki 3,000 zaidi wa Wagner ya Urusi

Jamhuri Ya Afrika Ya Kati Yatafuta Mamluki 3,000 Zaidi Wa Wagner Ya Urusi.png Jamhuri ya Afrika ya Kati yatafuta mamluki 3,000 zaidi wa Wagner ya Urusi

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Jamhuri ya Afrika ya Kati yatafuta mamluki 3,000 zaidi wa Urusi Tovuti ya Habari ya Corbeau inayounga mkono upinzani iliripoti jana kuwa Waziri Mkuu Felix Moloua ameomba kutumwa kwa mamluki 3,000 wa ziada wa Urusi ili kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usalama.

Waziri Mkuu aliliomba Kundi la Wagner kuongeza kikosi chao ili kusaidia jeshi kupambana na makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakitishia kuuteka mji mkuu, Bangui.

Ripoti hiyo inakuja siku moja baada ya mamluki wa Urusi kuanza kufanya doria za angani kufuatia tetesi za shambulio linalokaribia la Bangui na waasi wa Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC).

Idadi kamili ya mamluki nchini CAR haijulikani lakini Urusi inasema kuna wapiganaji 1,135 huku serikali ya Afrika ya Kati ikiweka idadi hiyo kuwa 5,000.

Wagner analiunga mkono jeshi la CAR kupambana na makundi mengi ya waasi ambayo yanadhibiti maeneo makubwa.

Chanzo: Bbc