Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jambazi sugu asukumwa jela miaka 5 baada ya kutubu dhambi kanisani

D67e51f8e31f7eb7 Jambazi sugu asukumwa jela miaka 5 baada ya kutubu dhambi kanisani

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Abraham Nduba, mwenye miaka 26, alikamatwa mwezi mmoja baada ya kukwepa mtego wa polisi

- Nduba alikiri kuwa mwanachama wa kundi la Gaica huku akitubu dhambi zake katika kanisa la Kiangilakana la Maragua

- Alishtakiwa na makosa matatu ya uhalifu, uuzaji wa pombe haramu na kumiliki kampuni ya kutengeneza pombe haramu

Mwanamume mmoja kutoka kaunti ya Murang'a amekamatwa na kutupwa jela miaka mitano baada ya kuungama kanisani kwamba ni mwanachama wa genge la uhalifu eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, Jumanne, Aprili 13, Abraham Nduba, mwenye miaka 26, alikamatwa mwezi mmoja baada ya kukwepa mtego wa polisi.

Nduba alikiri kuwa mwanachama wa kundi la Gaica huku akitubu dhambi zake katika kanisa la Kiangilakana la Maragua ambapo alikuwa amekwenda kuokoka.

Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Sivai Agade, siku ya Jumatatu, Aprili 4, ambapo alishtakiwa na makosa matatu ya uhalifu, uuzaji wa pombe haramu na kumiliki kampuni ya kutengeneza pombe haramu.

Nduba aliungama makosa yake na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani au faini ya KSh2 milioni.

Inaripotiwa kwamba Nduba alikwenda kanisani humo bila kufahamu kwamba alikuwa anaandamwa na kikosi kizima cha polisi.

Alifika kanisani akiwa mchangamfu, na tayari kumpokea Yesu Kristu kama mkombozi wa maisha yake bila kujua alikuwa ameketi pamoja na maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia.

Walimupa muda kutubu dhambi zake zote na kukubali kuishi maisha mapya kama pamba.

Punde baada ya ibada, pasta wa kanisa hilo Peter Kariuki aliarifiwa na polisi amsindikize Ndiba hadi katika Kituo cha Polisi cha Maragua ili ajisalimishe.

Pasta huyo alisimulia namna aliingiza baridi polisi walipomunyoshea bunduki na kuwaomba wamruhusu amwombee kondoo wake ambapo walikubali.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke