Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa atishia kuufukua mwili wa bintiye baada ya kuzikwa pasipo uwepo wake

E35727e6e1f53e08 Jamaa atishia kuufukua mwili wa bintiye baada ya kuzikwa pasipo uwepo wake

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Agrey Siema anasemekana hakuhudhuria mazishi ya mwanawe wa miaka 14 ambaye alizikwa siku ya Jumanne, Juni 30Kakake aliyetambulika kama Charles Musee alisema familia iliamua kuuzika mwili baada ya Siema kuondoka nyumbani bila kusema alikokuwa akielekeaKulingana na kakake, Siema alirejea nyumbani majira ya saa nane mchana baada ya bintiye kuzikwa Jamaa mmoja aliwaacha wakazi wa kijiji cha Kamwega eneo la Shinyalu na wasiwasi mkubwa baada ya kujaribu kufukua mwili wa binti yake.

Kwa mujibu wa taarifa za West FM, Aggrey Siema, 52, hakuwa nyumbani wakati bintiye wake wa miaka 14 alipozikwa siku ya Jumanne, Juni 30.

Kakake Siema alisema Charles Siema aliondoka nyumbani majira ya asubuhi lakini alirejea nyumbani kama bintiye ameshazikwa.

Siema alipogundua kwamba bintiye amezikwa pasipo uwepo wake, alianza kuzua rabsha na kuwafukuza waombolezaji.

" Siku ya Jumatano, familia ilimuzika bintiye lakini kakangu hakuwa karibu, aliondoka asubuhi na kisha kurejea mwendo wa saa nane mchana, alipata mwanawe akiwa tayari amezikwa. Alianza vurugu na kuanza kumfukuza kila mtu nyumbani kwake akiwemo mamake mkwe," Kakake alisema.

Kakake alipojaribu kuingilia kati, alimtishia kwamba angemkata kwa panga na kutaka mwili wa bintiye ufukuliwe na uzikwe kulingana tamaduni.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke