Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa ashtakiwa kwa kushindwa kulipa deni la Tsh. laki 7 hotelini

Cd10c5114b7aa7b0 Jamaa ashtakiwa kwa kushindwa kulipa deni la Tsh. laki 7 hotelini

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mfanyabiashara wa Nairobi, mnamo Ijumaa, alifikishwa mbele ya Mahakama ya Kibera kwa madai ya kukataa kulipa bili ya hoteli kwa vinywaji na chakula alichoagizia marafiki na wageni wake.

Benedict Nyanjong alishtakiwa kwa kukosa kulipa bili ya KSh 36,950 baada ya kujivinjari akiwa K1 Club House huko mtaani Parklands kulingana na ripoti ya K24.

Mshukiwa huyo anasemekana kwenda katika hoteli hiyo na kutumia Ksh 11,825 kununua vinywaji na marafiki zake walipoingia aliwaalika kwenye meza yake ili wajiburushishe pamoja

Kulingana na stkabadhi za mahakama, mshtakiwa alilipa Ksh 11,000 lakini alifahamishwa na hoteli kwamba bado anadaiwa Ksh 825 za pamoja.

Hata hivyo, aliendelea kuagiza chakula na vinywaji kwa ajili ya kuwaburudisha marafiki saba na wageni huku akisukuma bili yake hadi KSh 36,950.

Nyajong, hata hivyo, alikataa kulipa bili akidai kuwa hoteli hiyo imepandisha bei ya bidhaa zao.

Mvutano huo ulisababisha uongozi wa hoteli hiyo kuwaita polisi kuhusu ambao walimkamata mshtakiwa kwa kujiingiza katika gharama akijifanya ana pesa.

Alipofika kwa Hakimu Mkazi William Tulel, Nyajong alikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya KSh 80, 000 na KSh100, 000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 12.

Katika kisa sawia na hicho jamaa mwingine alifikishwa mahakamani Kibera ambapo alishtakiwa kwa kujipa bidhaa kwa mkopo kwa njia ya udanganyifu.

Evans Owino alishindwa kulipa bili ya KSh 6,710 baada ya kujivinanjari na wanawake kadhaaa kilabuni.

Wawili hao waliripotiwa kukutana Oktoba 5 kujivinjari Hacienda Sports Bar and Grill mtaani Westlands, Nairobi.

Owino alimvutia mwanamke huyo kwenye meza yake ambapo alikuwa akinywa bia na soda ya Krest.

Baada ya kusonga kwenye meza yake mwanamume huyo alianza kuitisha mlo na vinywaji wakati alijua hana pesa ya kugharamia.

Aliagiza aletewe vinywaji zaidi na nyama choma kufurahia na mwanamke huyo ambaye wakati huu sasa walikuwa marafiki.

Mmoja wa wahudumu aliona bili ya jamaa imekuwa kubwa akamtaka alipe.

Polisi walipigwa simu baada ya kubainika kwamba jamaa hangelipa bili ya hotelini humo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke