Mwanamume mwenye umri wa miaka 26, ambaye alikuwa kwenye misheni inayoshukiwa ya kutekeleza mauaji, aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akitembea kwenye mitaa ya Brooklyn jijini New York.
Gazeti la NewYork Post linaripoti kwamba mwanamume huyo, ambaye alikuwa amevaa glavu za mpira kwenda kutekeleza uhalifu huo, alipigwa risasi kichwani na mtu aliyekuwa akiendesha gari aina ya Sedan, polisi walisema Jumanne, Novemba 1.
Kulingana na polisi, mwathiriwa alikuwa amekamatwa mara kadhaa jijini humo, na polisi wanaamini kwamba alikuwa amepanga kufanya ufyatulianaji risasi na watu wengine wawili.
Alikimbizwa katika Kituo cha Matibabu cha Kings County, ambapo alithibitishwa kufariki dunia.