Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa ambaka mwanaye, ampa ujauzito

Aambaka Mwanaye Jamaa ambaka mwanaye, ampa ujauzito

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: TUKO

Polisi katika eneo la Rabuor Kaunti ya Kisumu wanamshikiliwa mwanamume mmoja wa miaka 42 kwa tuhuma za kumnajisi na kumpachika mimba binti wake wa kambo.

Polisi walisema kuwa mshukiwa alikamatwa katika kaunti ndogo ya Kadido baada ya walimu wa mwanafunzi huyo wa darasa la saba kugundua kuwa alikuwa ameanza kudhihirisha tabia zisizo za kawaida.

Baada ya kuhojiwa, msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 alipelekwa katika kituo cha afya kilicho karibu ambacho kilithibitishwa kuwa na ujauzito wa miezi minne.

Kwa mujibu wa naibu chifu wa kata ndogo ya Kapiyo Amos Odeny, mshukiwa tayari amepinga madai ya kuhusika na unajisi wa mtoto huyo.

Mtoto huyo amepelekwa katika nyumba iliyo salama. Mwanamume huyo ni baba wa kambo wa msichana. Alioa mamake kama mke wa pili,” Odeny alisema.

Chanzo: TUKO