Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa aliyekiri kumuua mpenziwe Catherine Nyokabi asema hana hatia

E82c7f78117c6625 Jamaa aliyekiri kumuua mpenziwe Catherine Nyokabi asema hana hatia

Wed, 5 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Evans Karani alifikishwa mbele ya Korti ya Kiambu Jumatano, Mei 5

- Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 38 alikanusha kumuua Catherine Nyokabi ambaye alisemekana kuwa mpenzi wake wa kando

- Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana huko Witeithie baada ya wakaazi kuripoti kuhusu gari lililokuwa limekwama kwenye Barabara ya Bob Harris huko Juja

Jamaa mwenye umri wa miaka 38 ambaye alikiri kumuua mpeni wake amefunguliwa mashtaka.

Evans Karani alifikishwa mbele ya Korti Kiambu Jumatano, Mei 5, ambapo alikanusha kumuua Catherine Nyokabi, ambaye alisemekana kuwa mpenzi wa pembeni.

Jaji Mary Kasango aliarifiwa kwamba Karani anadaiwa kutenda kosa hilo Jumanne, Aprili 13, katika eneo la Witeithie katika kaunti ya Kiambu.

Ingawa mshukiwa aliomba la kuachiliwa kwa dhamana, jaji alisema korti haikuwa na uwezo wa kutoa uamuzi ikiwa mshtakiwa anapaswa kupewa matakwa yake.

Mahakama itakuw ana kikao kingiine Ijumaa, Juni 2, kuamua hatima ya Karani.

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana huko Witeithie baada ya wakaazi kuripoti kuhusu gari lililokuwa limekwama kwenye Barabara ya Bob Harris huko Juja.

Mita chache kutoka eneo mbalo gari hilo lilikuwa limekwama mwili wa dada huyo ulipatikana.

Makachero walishuku kwmaba huenda mshukiwa alipanga kuutupa mwili wa msichana huyo mahali kwingine lakini juhudi zake zilisambaratika baada ya gari hilo kumwama kwenye tope.

Baadaye kutokana na uchungiz wao wa kina polisi walimfumania Karani mafichoni mtaani Githurai.

Karani ambaye ana mke alikiri kwamba alimuua mpenzi wake huyo Nyokabi.

Kwenye kikao kilichoandaliwa Jumatatu, Aprili 19 mshukiwa alimuarifu hakimu mkaazi Osacr Wanyaga kumharakishia hukumu yake ndiposa aanze na mapema kutumikia jela.

"Nauliza ikiwa unaweza kufanya uamuzi wako haraka iwezekanavyo ili nianze kifungo changu mapema ," alisema.

Hata hivyo hakimu alimuarifu kwamba ni lazima asubiri kwa muda kesi kufanywa kisha ikamilishwe kabla ya hukumu kutolewa.

"Bado sijatoa uamuzi wengu, unanielewa?" hakimu alimuuliza Karani ambaye alisema angengojea kuhukumiwa kwake.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke