Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa aliyechanganyikiwa azuia gari la Rais Uhuru Lucky Summer

045ec33ea21ba3af Jamaa aliyechanganyikiwa azuia gari la Rais Uhuru Lucky Summer

Thu, 27 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wakazi wa Lucky Summer waliduwaa baada ya jamaa asiyejulikana kusimama mbele ya gari la Uhuru

- Baada ya kisa hicho cha Jumatano, Mei 26, kulikuwa wasiwasi kuhusu usalama wa kiongozi wa taifa

- Hata hivyo, Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna aliondoa wasiwasi hiyo akisema mwanamume huyo mwenye umri wa kati alikuwa na furaha kumuona kiongozi huyo wa Chama cha Jubilee

Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna amepuzilia mbali madai kuwa usalama wa Rais Uhuru Kenyatta umo hatarini baada ya jamaa kuzuia gari lake Lucky Summer.

Baada ya kisa hicho cha Jumatano, Mei 26, kulikuwa wasiwasi kuhusu usalama wa kiongozi wa taifa.

Hata hivyo, Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna aliondoa wasiwasi hiyo akisema mwanamume huyo mwenye umri wa kati alikuwa na furaha kumuona kiongozi huyo wa Chama cha Jubilee.

"Mnamo Mei 26, 2021, jamaa mmoja alisimama mbele ya msafara wa Rais wakati wa ziara yake katika mtaa wa Lucky Summer, kaunti ya Nairobi. Jamaa huyo ni raia ambaye alikuwa tu na furaha kuona msafara wa Rais Uhuru Kenyatta. Tungependa kuondoa wasiwasi wowote kuhusu usalama wa Rais kuwa hatarini," alisema Oguna.



Jamaa huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamepiga foleni katika mtaa wa Gathecia kutazama msafara wa rais ukitokea Neema abattoir.

Ghafla bin vuu alisimama kati kati ya barabara kuashiria gari la Uhuru lisimame.

Hii ilipelekea maafisa wa usalama wa rais kumuondoa mchakamchaka barabarani kabla ya rais kuendela na safari yake.

Wiki moja iliyopita, maafisa wa usalama walimsukuma mwanamume mmoja aliyekuwa anajaribu kusonga karibu na kiongozi wa taifa akihutubia wakazi wa kaunti ya lamu.

Katika video iliyosambaa, Uhuru aliyepigwa na butwaa, alikatiza hotuba yake kwa muda huku mlinzi wake akikabiliana na jamaa huyo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke