Wasafiri wanaotumia stendi ya mabasi Kisumu nchini Kenya wameachwa na mshangao mkubwa baada ya mwanamume mmoja kuzimia na kufariki dunia katika hali isiyoeleweka.
Roy Onyango aliyetambulika kama Ngala alianguka katika katika ya mabasi ghafla ambapo yeye hufanya kazi ya kupakia mizigo. Marahemu alikuwa akiwasimulia hadithi jamaa ambao yeye hufanya kazi nao.
Akizungumza na Citizen TV, afisa wa kituo hicho, Ochieng Omwa, alisema walijaribu kumkimbiza hospitalini haraka lakini walikuwa wameshachelewa.
Wakati wakimkimbiza katika hospitali ya karibu, tayari alikuwa ameacha kupumua. “Ngala alikuwa mchangamfu, asubuhi na alikuwa akizungumza na wapakiaji wenzake lakini kifo chake cha ghafla kimeacha watu vinywa wazi,” alisema Omwa.
Polisi waliokuwa wakipiga doria katika stendi hiyo walimpeleka Onyango kwenye chumba cha kuhifadhia maiti wakisubiri uchunguzi wa maiti kufanywa.