Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalang'o kuwania kiti cha ubunge cha Lang'ata 2022

Ec45940fae21c1ce Jalang'o kuwania kiti cha ubunge cha Lang'ata 2022

Fri, 16 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Katibu Mkuu wa Chama cha ODM amemkaribisha Jalang'o katika chama hichoJalang'o alitangaza awali kwamba atawania kiti cha ubunge cha Lang'ata katika uchaguzi mkuu wa 2022Tayari Jalang'o amepokezwa cheti cha uananchama na Sifuna ingawa mwenyewe hajathibitisha rasmi iwapo atakuwa debeniMtangazaji wa kituo cha redio cha Kiss 100 na mchekeshaji maarufu Jalang'o amejiunga na chama cha ODM huku uchaguzi mkuu wa 2022 ukikaribia.

Jalang'o alikuwa ametangaza awali kwamba atawania kiti cha ubunge cha Lang'ata lakini hakuonyesha shinikizo lolote.

Katibu wa chama hicho Edwin Sifuna sasa amefichua kwamba Jalang'o ni mwanachama halali wa chama hicho na atawania kiti cha ubunge cha Lang'ata katika uchaguzi mkuu wa 2022.

" Leo Jalang'o alijiunga na chama kikubwa nchini, alipokezwa cheti cha uanachama na katibu mkuu wa chama hicho,Tuko tayari kufanya kazi kwa pamoja," Sifuna alisema.



Read also

Raila Hatapewa Tiketi ya Moja kwa Moja Kuwania Urais, ODM Yasema

Taarifa hii inajiri saa chache baada ya Sifuna kuhojiwa na Televisheni ya Jalang'o maarufu Jalang'o TV siku ya Alhamisi, Julai 15.

Hata Hivyo, Jalang'o hajatangaza mwenyewe iwapo atakuwa kwenye debe ifikapo 2022.

Kando na hayo, Jalang'o amekuwa akisifiwa na wanamitandao kwa juhudi zake za kuwasaidia Wakenya wasiojiweza.

Wa hivi punde alikuwa Harun Gitari ambaye alifanikisha safari yake ya kwenda India kwa ajili ya matibabu.

Gitari aligonga vichwa vya habari mwaka wa 2020 baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa ajabu ambao umefanya vidole vyake vya mikono kujikunja na kufura.

Hata hivyo amepata afueni baada ya Jalang'o kuchangisha fedha za kugharamia matibabu yake huku gavana Joho akimlipia tiketi ya ndege pamoja na kakake aliyeandamana naye.

Jalang'o aliwashukuru Wakenya wengine walihusika katika kufanikisha safari ya Gitari ya kwenda India.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.



Read also

Jalang'o Afurahia Baada ya Kumsaidia Mgonjwa Kusafiri Kwenda India kwa Matibabu
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke