Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji wa Uganda achukua wadhfa wa makamu wa rais wa mahakama ya kimataifa ICJ

Jaji Wa Uganda Achukua Wadhfa Wa Makamu Wa Rais Wa Mahakama Ya Kimataifa ICJ Jaji wa Uganda achukua wadhfa wa makamu wa rais wa mahakama ya kimataifa ICJ

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Jaji mzaliwa wa Uganda Julia Sebutinde amechaguliwa kuwa makamu wa rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iliyoko Hague, Uholanzi.

Jaji huyo hivi majuzi alizua utata katika jumuiya ya kimataifa alipotoa uamuzi dhidi ya hatua za dharura zilizoombwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu vita vya Gaza.

Alikuwa jaji wa pekee katika jopo la wanachama 17 wa ICJ kupiga kura dhidi ya hatua zote sita zilizopitishwa na mahakama ya ICJ katika uamuzi ulioamuru Israel ichukue hatua ya kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki inapopambana na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Bi Sebutinde alikuwa mmoja wa majaji wawili pekee waliotoa hukumu zilizopingana huku 15 wakipigia kura hatua za dharura ambazo zilishughulikia mengi ya yale ambayo Afrika Kusini iliomba katika kesi hiyo.

Serikali ya Uganda ilijitenga na maoni pinzani ya jaji, ikisema hawakilishi msimamo wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika mzozo huo.

Kulikuwa na maoni mengi ya ukosoaji kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakishangaa ni kwa nini alichagua kutokuwa na huruma zaidi na kesi ya Afrika Kusini.

Mahakama ilitangaza Jumanne kwamba Bi Sebutinde alichaguliwa kuwa makamu wa rais kwa miaka mitatu, katika kile kinachoonekana kuwa kura kubwa ya imani naye.

Jaji mzaliwa wa Lebanon Nawaf Salam anachukua nafasi ya jaji-rais wa ICJ kutoka Joan Donoghue.Bi Sebutinde amekuwa jaji wa ICJ kwa zaidi ya muongo mmoja.

Hapo awali aliendesha kesi kadhaa za uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashtaka kwa Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.

Chanzo: Bbc