Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji nchini Kenya aagiza wanaume kuwalipa mishahara wake zao

Jaji MATHEKA.jpeg Jaji nchini Kenya aagiza wanaume kuwalipa mishahara wake zao

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

JAJI Mkuu wa Kenya Theresia Matheka wiki iliyopita ametoa hukumu inayosema Wanawake walioolewa na kubaki kuwa Mama wa nyumbani ni kazi kama kazi nyingine (na wala sio ugolikipa) na kusema Wanaume wanastahili kuwalipa mshahara Wake zao hao.

Jaji amesema ingekuwa sio jambo jema kwa Mahakama kutoa maamuzi ya kwamba Mama wa nyumbani hana mchango wowote kwenye Familia hususani wa kifedha, alisema hayo wakati akitoa uamuzi wa kesi ya Mwanamke aliyelalamika Mumewe kuuza vitu vyote walivyotafuta pamoja akidai Mwanamke hajachangia kitu maana hakuwa na kazi.

“Kulea Watoto, kupika na kusafisha nyumba ni kazi kubwa ambapo familia nyingine zinawalipa wadada wa Kazi kusaidia hizo kazi, sasa mwanamke anayeshinda nyumbani akifanya kazi hizi zote na kumuhudumia mwanaume pia anapaswa kulipwa mshahara kabisa na Mumewe kama Wafanyakazi wengine badala ya kusema hana mchango wowote kisa hafanyi kazi,” alisema Jaji Matheka.

Chanzo: globalpublishers.co.tz