Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mkuu wa kwanza wa kike Zambia, Irene Mambilima aaga dunia

9b8f76d323f61fc0 Jaji Mkuu wa kwanza wa kike Zambia, Irene Mambilima aaga dunia

Mon, 21 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Jaji Mkuu Irene Mambilima aliaga dunia nchini Misri Jumapili, Juni 20, akiwa katika ziara rasmi Kulingana na taarifa ya katibu wa Rais wa Zambia, Edgar Lungu, Simon Miti jaji huyo alianza kuugua akiwa nchini humo na kisha kufarikiJaji Mambilima alisimamia chaguzi kuu za mwaka 2006 na 2011 ambapo chama tawala cha sasa PF kiliondoa MMD madarakani

Jaji Mkuu wa kwanza wa kike nchini Zambia, Irene Mambilima ameaga dunia akiwa katika ziara rasmi Misri baada ya kuugua ghafla.

Taarifa kuhusu kifo chake ilithibitishwa na shirika la habari la serikali ya Zambia ambalo lilisema Mambilima aliaga dunia Jumapili, Juni 2.

Kulingana na taarifa ya katibu wa Rais wa Zambia, Edgar Lungu, Simon Miti jaji huyo alianza kuugua akiwa nchini humo na kisha kufariki

“Tunasikitika kutangaza kuwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Chagwa Lungu anatangaza kifo cha ghafla cha Jaji Mkuu Irene Chirwa Mambilima, Zambia kilichotokea leo Jumapili, Juni 20, 2021, katika hospitali moja ya kibinafsi jijini Cairo, Misri," ilisoma taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilifichua kuwa, Mambilima alisafiri jijini Cairo mnamo Juni 10 2021, kwa shughuli rasmi na alifariki akiwa kazini nchini humo.

Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 69 na aliapishwa mwaka 1977.

Itakumbukwa kuwa Jaji Mambilima aliidhinishwa kuwa Jaji Mkuu mnamo Februari 26, 2015 na kuibuka jaji mkuu wa kwanza wa kike nchini Zambia.

Kabla ya uteuzi wake kuwa Jaji Mkuu, Mambilima alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ).

Akiwa katika wadhifa huo, Jaji Mambilima alisimamia chaguzi kuu za 2006 na 2011 ambapo chama tawala cha sasa PF kiliondoa MMD madarakani.

Alifuzu na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na Shahada ya Uzamili Kutoka Chuo Kikuu cha London.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka TUKO

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke