Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mkuu wa Tunisia afafanua sakata la Mahakama kuwa kinyume na sheria

Jaji Tunisia Jaji Mkuu wa Tunisia afafanua sakata la Mahakama kuwa kinyume na sheria

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaji mkuu nchini Tunisia Youssef Bouzakher leo amemshtumu rais wa nchi hiyo Kais Saied kwa kuhujumu uhuru wa idara ya mahakama kwa kuvunjilia mbali baraza kuu la mahakama na kuonya kuwa majaji hawatakaa kimya.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Bouzakher amesema kuwa hilo ni jaribio la kuwaweka majaji hao chini ya maagizo ya rais na kuongeza kwamba uamuzi huo wa rais ni kinyume na sheria.

Rais Saied alitangaza uamuzi huo jana usiku hii ikiwa hatua ya hivi karibuni zaidi ya kuimarisha madaraka baada ya kulivunja bunge nakumsimamisha kazi waziri mkuu mwezi Julai na kuahidi kufanyia marekebisho katiba ya kidemokrasia katika hatua ambazo wakosoaji wake wanaziita mapinduzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live