Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Mkuu Kenya ateua majaji watatu kesi sheria ya fedha

Jaji Mkuu Kenya Ateua Majaji Watatu Kesi Sheria Ya Fedha.png Jaji Mkuu Kenya ateua majaji watatu kesi sheria ya fedha

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Jaji Mkuu Martha Koome ameteua benchi la majaji 3 kusikiliza na kuamua malalamishi ya kupinga Sheria ya Fedha ya 2023.

Majaji hao watatu ni Lawrence Mugambi, David Majanja na Christine Meori.

Benchi ambayo inaongozwa na David Majanja inatarajiwa kubainisha kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah na wengine sita.

Walihamia kortini kutaka sheria hiyo mpya itangazwe kuwa kinyume na katiba wakisema kuwa Sheria ya Fedha ya 2023 haikuwa halali kwa vile mswada huo haukupitishwa katika Seneti kama inavyotazamiwa na sheria.

Waliteta kuwa hakuna maelewano ya Maspika wa Bunge la Kitaifa na Seneti kuhusu masuala yanayohusu kaunti.

Jaji wa Mahakama ya Juu Mugure Thande alisimamisha kwa muda utekelezaji wa Sheria ya Fedha mnamo Juni 30.

Mnamo Julai 10, hakimu aliidhinisha kusimamishwa kwake, akishikilia kusitishwa kwa utekelezaji wake.

Serikali ilikuwa na matumaini ya kuongeza mapato zaidi ili kufadhili bajeti yake ya Sh3.6 trilioni lakini hatua hizo mpya za ushuru huenda zisiafikiwe baada ya Mahakama Kuu kukataa kuondoa maagizo yaliyositisha utekelezwaji wa ushuru huo mpya.

Majaji hao watatu watapanga tarehe ambayo shauri hilo litatajwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Mwanaharakati Okiya Omtatah na wengine wanne waliwasili mahakamani mwezi uliopita ili kupinga mswada wa fedha unaopendekezwa 2023.

Kulingana na dua lao, wanapinga kwamba mswada huo utakuwa unazidhalilisha haki ya binadamu za kiuchumi kisha kuchangia gharama kubwa katika baadhi ya bidhaa iwapo mswada huo utafanywa kuwa sheria.

“Inasubiri kusikilizwa na mahakama itakuwa radhi kutoa amri ya kusitisha mjadala kulingana na vipengele 28,30,33,36 na 76 vya mswada wa fedha mwaka wa 2023.” Akisoma karatasi za mahakama.

Chanzo: Radio Jambo