Nairobi, Kenya. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Sankale Ole Kantai ameingia katika kashfa ya kushirikiana na mtuhumiwa wa mauaji ya bilionea wa Kenya, Tob Cohen.
Bilionea huyo raia wa Uholanzi aliuawa mwishoni mwa mwaka jana kisha mwili wake kufukiwa katika shimo la choo nyumbani kwake jijini Nairobi.
Tukio hilo linadaiwa kufanywa na aliyekuwa mke wa bilionea huyo, Sara Wairimu ambaye sasa yuko rumande akikabiliwa na kesi ya mauaji.
Taarifa ya polisi ilisema Jaji Kantai atafikishwa mahakamani wakati wowote kufuatia madai ya kushirikiana na mshukiwa huyo wa mauaji.
Taarifa hiyo ilisema Jaji Kantai alikamatwa na maofisa wa polisi Ijumaa iliyopita na kuhojiwa kuhusu uhusiano wake na mwanamke huyo ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo, jaji huyo aliyelala kwa siku moja katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga jijini Nairobi, aliachiwa Jumamosi mchana kwa dhamana.
Pia Soma
- Dk Bashiru asema hatima ya Membe, Kinana na Makamba kujulikana kabla ya Machi 2020
- Madiwani 11 wa CCM Mbeya wahama Chadema, Dk Bashiru amtumia salamu Sugu
- Kabendera akiri makosa, ahukumiwa kulipa fidia na faini zaidi ya Sh270 milioni
- Kabendera atiwa hatiani kwa mashtaka mawili
Kwa mujibu wa Idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai Kenya, jaji huyo atashtakiwa kwa tuhuma za kula njama ya kuingilia mashahidi.