Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jacob Zuma kutupwa jela kwa miezi 15, akashifiwa kwa kukiuka amri ya korti

0fgjhs2hi0cac8p0c Jacob Zuma kutupwa jela kwa miezi 15, akashifiwa kwa kukiuka amri ya korti

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amehukumiwa kifungo cha miezi kumi na tano gerezani na mahakama kuu nchini humo.

Zuma anakashiwa kwa kuhusika katika ufisadi wakati alipokuwa madarakani.

Kulingana na korti ya Katiba nchini humo, Zuma amekuwa akikaidi amri ya mahakama kwa mara kadhaa.

Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama, Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza kesi ya Zuma, aliiomba mahakama itangaze kwamba rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.

Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka wa 2018, Zuma amekuwa akikanusha shutuma za ufisadi ambazo zinamkabili.

Hapa Kenya, baaadhi ya viongozi akiwemo seneta mteule Millicent Omanga wamefurahishwa na hatua ya kukamatwa kwa Zuma.

Kulingana na Omanga huenda Rais Uhuru akafuata mkondo huo huo.

Omanga alidai kwamba Uhuru hajakuwa akiheshimu amri za mahakama na kwa hivyo anapaswa pia kutupwa jela.

" Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alipatikana na hatia ya kukaidi amri ya korti, mtupe jela kwa muda wa miezi kumi na tano na kwa wale ambao wanazidi kukiuka amri ya mahakama kwa sababu eti wako kwenye madaraka wachukulie jambo hili kwa uzito, wakati wao unakuja," Omanga alisema.

Zuma alikuwa ametakiwa kufika katika kituo cha polisi kilicho karibu na nyumbani kwake mjini Nkandla lakini hakufanya hivyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke