Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jacob Zuma kutumikia kifungo nyumbani

ZUMA?fit=620%2C372&ssl=1 Jacob Zuma, Rais wa zamani wa Afrika Kusini

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya kukaidi agizo la Mahakama kuhusu kesi ya rushwa dhidi yake, ameruhusiwa kumaliza kifungo chake akiwa nyumbani kutokana na kuumwa kwake.

Idara ya Magereza imetangaza msamaha huo wa kiafya miezi miwili tu tangu Zuma (79) aanze kutumikia kifungo hicho ambapo amelazwa katika hospitali moja nje ya Mahakama hiyo tangu August 6.

August 14 alifanyiwa upasuaji ambao hadi sasa hIjaelezwa ulikua wa nini ila Idara ya Magereza imesema kwamba uamuzi huu mpya ulitokana na ripoti ya kiafya waliyopata kuhusu Zuma, hata hivyo wamesema atahitajika kufuata masharti atakayopewa na watamfuatilia kuhakikisha anamaliza kifungo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live