Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jacob Zuma alazwa hospitali kwa uchunguzi

Jacob Zuma Rais wa zaman wa Afrikakusini Jacob Zuma

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: Bbcswahili

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa katika hospitali nje ya gereza kwa ajili ya kufanyiwa uangalizi wa kimatibabu, wamesema maafisa wa gereza.

Wakfu wake umesema kuwa ulikuwa ni "uchunguzi wa kawaida wa kimatibabu wa kila mwaka" na kwamba "hakuna lolote la kutisha".

Kama rais wa zamani wa nchi, Zuma anatibiwa katika hospitali ya jeshi, maafisa wamesema.

Rais huyo wa zamani amekuwa akitumikia kifungo cha miezi 15 gerezani tangu alipohukumiwa tarehe 7 Julai kwa kutoheshimu agizo la mahakama.

Maafisa wa gereza wanasema kuwa ana haki ya kupata matibabu kama mfungwa mwingine yoyote yule anayefungwa gerezani.

Chanzo: Bbcswahili