Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jacob Zuma achoka kutiliwa mashaka juu ya afya yake

Zuma123.jpeg Jacob Zuma, Rais wa zamani wa Afrika Kusini

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ameishutumu Mahakama kwa kutoamini ripoti ya kitabibu huku akikataa kufanyiwa uchunguzi na daktari aliyechaguliwa na mamlaka ya mashtaka.

Malalamiko hayo yanakuja mara baada ya Madaktari kuwasilisha ripoti ya siri juu ya afya ya Bwana Zuma kuwa anamudu kuhudhuria kesi yake.

Msemaji wa Familia ya Zuma, Mzwanele Manyi, aliiambia runinga ya ENCA kuwa Rais huyo wa zamani amechoka kitendo cha kutiwa mashaka juu ya afya yake.

Rais huyo alilazwa hospitalini siku chache baada ya kukamatwa na kufanyiwa upasuaji tarehe 14 mwezi Agosti, na hivi sasa anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kosa la kudharau Mahakama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live