Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jacob Zuma aahidi kujenga viwanda na kutoa elimu ya bure kwa vijana

Jacob Zuma Aondolewa Hukumu Ya Kifungo Cha Miaka 15 Yaondolewa Jacob Zuma aahidi kujenga viwanda na kutoa elimu ya bure kwa vijana

Mon, 20 May 2024 Chanzo: Voa

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma Jumamosi alilalamika juu ya viwango vya juu vya umaskini miongoni mwa waafrika Kusini weusi na kuahidi kubuni nafasi za kazi na kukabiliana na uhalifu alipokuwa akizindua ilani ya chama chake kipya cha kisiasa kabla ya uchaguzi unaotarajiwa nchini humo.

Aliwaambia maelfu ya wafuasi waliokusanyika katika Uwanja wa Orlando mjini Johannesburg kwamba chama chake kitajenga viwanda ambapo watu wengi wataajiriwa na kutoa elimu ya bure kwa vijana wa nchi hiyo.

Tunataka watoto wetu wasome bure, hasa wale wanaotoka katika kaya maskini kwa sababu umaskini tulionao haujatengenezwa na sisi. Ulisababishwa na walowezi ambao walichukua kila kitu, pamoja na ardhi yetu. Tutarudisha vitu hivyo vyote, tupate fedha na kusomesha watoto wetu,” alisema.

Pia ameahidi kubadili Katiba ya nchi ili kurejesha mamlaka zaidi kwa viongozi wa kimila, akisema nafasi yao katika jamii imepunguzwa kwa kuwapa mamlaka zaidi mahakimu na majaji.

Chanzo: Voa